Bunge la Tanzania linaanza vikao vyake wiki ijayo, moja ya ishu ambayo wanasiasa na wanaharakati mbalimbali wamekuwa wakishinikiza kufanyiwa maamuzi ni ishu ya Escrow, mwezi DECEMBER, 2014 Rais Kikwete alitangaza kumsimamisha kazi Waziri Anna Tibaijuka kutokana na ishu ya fedha za Escrow ambazo kulikuwa na utata kwamba ni za umma ama za IPTL.
Vuguvugu lililobaki likawa kuwawajibisha Prof. Muhongo pamoja na Wenyeviti watatu wa Kamati za Bunge ambao walitajwa pia kuingiziwa pesa hizo, leo Prof. Muhongo ameitisha kikao na waandishi wa Habari ofisini kwake na kutangaza kujiuzulu nafasi ya Uwaziri.
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo ametangaza kujiuzulu leo January 24 kutokana na Ishu ya Escrow. Via: #ITV
— millardayo.com (@millardayo) January 24, 2015
Anakuwa Waziri wa pili kujiuzulu huku kukiwa na taarifa Magazetini leo kwamba Wenyeviti wa Kamati za Bunge nao pia wameachia nafasi hizo ili wachaguliwe wengine kabla ya Bunge kuanza Jumanne wiki ijayo.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook