Wakati Kikao cha Bunge kikiendelea Dodoma leo, miongozo bado iliendelea kuombwa na baadhi ya Wabunge kuhusiana na suala ambalo limechukua siku kadhaa sasa kwamba Mahakama ilitoa agizo la kuzuia Bunge kujadili kuhusiana na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu Wa Serikali CAG, leo Novemba 26 Wabunge Suleiman Nchambi, Esther Bulaya, Tundu Lissu, Ole Sendeka na Joshua Nassari waliomba mwongozo kuhusiana na hilo.
Mbunge Nchambi alianza kwa kuuliza; “… Watanzania waelewe wazi sisi wabunge wa Chama cha Mapinduzi tunayo dhamira ya kujadili jambo hili Bungeni na kwa kuwa CHADEMA wameonyesha waziwazi kupitia mjumbe wao kuwa wanapinga suala hili, naomba mwongozo wako kwanini wakati tunajadili suala hili zito tusijadili pia suala hili zito la mjumbe wa CHADEMA kwenda kupinga kujadiliwa hoja hiyo hapa Bungeni…”
Tundu Lissu akajibu hoja hiyo; “… Anaitwa Gabriel Mnyele, mkazi wa Mpanda ni mwana-CCM na wasiofahamu mimi nimesoma naye… Wakili wa Pan African Power Solutioms anafanya kazi kwenye kampuni moja ya uwakili na Mabere Marando, isipokuwa Wakili Mabere Marando hajahusika kwa namna yoyote ile na kesi iliyopelekwa Mahakamani...”
“… Kilichotokea jana kwa Mahakama Kuu kutoa amri kuzuia mjadala Bungeni, ni jambo ambalo halijawahi kutokea tangu Mahakama kuu ya Tanganyika ianzishwe mwaka 1922…“– Tundu Lissu.
Mwenyekiti wa Bunge Mussa Azzan Zungu amejibu haya kwenye miongozo iliyoombwa na Wabunge hao; “… Taarifa ya kiti ambayo ndiyo taarifa rasmi bado Bunge halijapokea barua yoyote ya kukataza mjadala wa Escrow kujadiliwa Bungeni. Hii miongozo mingine nitaijibu jioni.
Baada ya hapo Bunge liliahirishwa, na kupitia mtandao wa Twitter na Instagram, Mwenyekiti wa PAC Zitto Kabwe ameandika kwamba Ripoti hiyo itasomwa leo jioni katika kikao cha Bunge hilo.
Instagram : “Ripoti tayari inasubiri kuwasilishwa“– @zittokabwe
Twitter : “Taarifa ya PAC kusomwa saa kumi na moja jioni Leo“–Zitto Ruyagwa Kabwe @zittokabwe
Kuusikiliza mjadala huo wa Bunge bonyeza play hapa.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook