Kabla ya dirisha la usali la LIgi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019 kufungwa kulikuwa na taarifa kuwa club ya Singida United kupitia kwa Rais wa club hiyo Dr Mwigulu Nchemba walitoa wachezaji bure kwenda Yanga SC akiwemo Elisha Mroiwa raia wa Zimbabwe kabla ya Yanga baadae kumkataa.
Baada ya maamuzi hayo baadhi ya wachambuzi wa soka na wadau walikuwa wanapinga na kudai kuwa Singida United ni tawi la Yanga kutokana na Rais wao Dr Mwigulu Nchemba kuwa shabiki wa Yanga, mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga amelizungumzia hilo leo hii na msimamo wao wa kama club.
“Kwenye usajili huu watu wamekuwa na sintofahamu kuhusiana na Singida United kama timu ndogo inajitutumua kwenda kutoa wachezaji bure kwenda Yanga, waandishi wa habari na wadau wa soka walikuwa wanaona hili linaondoa ushindani katika Ligi”
Haji Manara haishiwi maneno “Kabla ya kunitolea povu nipinge kwa data”