Watu mbalimbali kutoka Dar es salaam na maeneo mengine ya Mkoa wa Mbeya walijitokeza kumzika Agness Geral Waya ‘Masogange’ wakiongozwa na Mkuu wa mkoa huo, Amos Makalla.
Akizungumza katika mazishi hayo, Makalla amesema hakuna mtu anayejiandaa wala aliye tayari kwa ajili ya kifo, hivyo kifo cha Masongange ni kielelezo kwamba binadamu wote hapa duniani ni wasafiri.
“Kifo cha Masogange kitukumbushe kwamba sote tutakufa, nimefurahi namna wasanii mlivyojipanga bila kujali bifu na tofauti zenu, katika hili mmekuwa pamoja, nilikuwa nafuatilia tangu msiba huu ulipotokea, mlikuwa pamoja na kwa mshikamano na sisi Serikali tunawapa pongezi sana” amesema Makalla.
MSIBA WA MASOGANGE: BELLE 9 AMESHINDWA KUONGEA MSIBANI