Mamia ya wakazi wa Bunju Dar es salaam wameshikwa na simanzi baada ya mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Bunju B kuangukiwa na mkorosho wakati akicheza na wenzake katika eneo la Shule na kufariki.
Wakiongea na kituo cha ITV mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema ; “… Majira ya saa nne kasoro Mwalimu alikuja kunipa taarifa kwamba kuna ajali imetokea baada ya kufika eneo la tukio nikaambiwa kwamba Mwanafunzi aliyeangukiwa na mti na amefariki hapo hapo na wasamaria walisaidia kumtoa katika hilo gogo alilokuwa ameangukiwa lakini nilikuta alikuwa kashatolewa pale kwenye eneo na amefunikwa…”
Shuhuda mwingine wa tukio hilo amesema “…Ni msiba mkubwa ambao umetukuta ni mpango wa Mungu, lakini pamoja na mpango wa Mungu naweza ukaona mazingira ya Shule yalivyo kuna vichaka hivi vichaka kuna mikorosho iliyoanguka, haikuanguka moja kwa moja imebaki nusu kamati za shule zipo, ilikua kazi za kamati ya shule ili kumalizia hiyo miti na mazingira ya Shule yakafyekwa kukawa kuzuri, sababu licha ya hiyo miti kuna nyoka, kuna watu amabao hawana nia nzuri wanaweza kukaa na wakachukua watoto, lakini kamati ya Shule imekaa kimya na wapo Mwenyekiti, Katibu na Wajumbe wake wito wangu mimi ni kwamba ikiwezekana kamati ya Shule wajipime waone kama inawezekana waachie ngazi...”
Naye kiongozi wa kamati ya Mazingira shuleni hapo amesema; “… Tutatafuta watu ambao wanakatakata mkaa ili tukae nao pamoja waanze kuipunguza kwa sababu tumeshaiona hatarishi kipindi kirefu kwa hiyo tushaamua suala hilo nafikiri baada ya muda fulani tutanza kulishughulikia…”
Kuisikiliza taarifa niliyoirekodi wakati kituo cha ITV kikirusha taarifa hiyo bonyeza play hapa.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook