Tanzania imepata ugeni kutoka kwa moja kati ya wachezaji soka wa Afrika wanaocheza soka la kulipwa England Wilfred Bony ambaye leo alikutana na waandishi wa habari, Wilfred Bony raia wa Ivory Coast amewahi kucheza vilabu mbalimbali Ulaya ikiwemo Man City na Swansea City ambayo anaitumikia kwa sasa.
Kama utakuwa unalumbuka vizuri Yaya Toure ambaye alikuwa anaichezea Man City baada ya kuondoka alinukuliwa na vyombo vya habari akimlalamikia kocha Pep Guardiola kuwa ana ubaguzi, leo baada ya kumpata Wilfred Bony tukamuuliza vipi kwa upande wake alicheza Man City na baadae kutopata nafasi sana na kutosha na kuondoka katika timu baada ya ujio wa Pep Guardiola.
Vipi anakubaliana na kauli ya Yaya Toure kuwa Pep Guardiola anawabagua wachezaji wa kiafrika, vipi kwa upande wake yeye?
“Yaya anamjua Guardiola zaidi kuliko mimi walikuwa pamoja Barcelona na mimi nimekaa na Guardiola kwa miezi miwili na tulikuwa na wakati mzuri na kila mmoja anamuheshimu mwenzake lakini mpira ni mpira sitaki kuingia katika hiyo hoja maana sijui nini kilitokea kati yao”
“Siwezi kusema ubaguzi wa rangi mimi haunigusi hapana ili ni tatizo ambalo anakutana nalo kila muafrika kiukweli kwa mimi siwezi kutia hata neno la kumtemtea mmoja kati yao kwa sababu siwezi kujua kilitokea nini kati yao na pia mimi haijawahi kunitokea hali hiyo ya kubaguliwa na yeye”
Haji Manara kapenda usiku wa VPL ila kafunguka wasiwasi wake