Shirikisho la soka Tanzania TFF leo limetangaza kumuadhibu mjumbe wao wa kamati ya utendaji ya shirikisho hilo na msimamizi wa kituo cha Shinyanga Mbasha Matutu, TFF imetoa taarifa rasmi ya kumfungia kupitia ukurasa wake wa instagram.
“Kamati ya Maadili iliyokutana Jumamosi Agosti 25,2018 Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) imemfungia kutojishughulisha na Mpira wa Miguu maisha”
“Aliyekuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na msimamizi wa kituo cha Shinyanga Mbasha Matutu kwa makosa matatu ya kushindwa kutekeleza majukumu yake,ubadhirifu,kughushi na kuiba kinyume na kanuni za Maadili na Ligi Kuu”
Samatta hataki utani safari ya Europa League, leo kapiga hat-trick