Boti mbili walizokuwa wakisafiria wahamiaji haramu kutoka Afrika Magharibi kwenda Ulaya zimepata ajali na kuzama katika bahari ya Mediterrania ambapo wahamiaji hao walikuwa wakijaribu kuzamia kwenda Ulaya.
Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR limesema ni watu nane pekee ndio walioweza kuokolewa baada ya kukaa majini kwa siku nne huku wengine 203 kutojulikana waliko ambapo taarifa zinasema wanahisi huenda watu hao wote wamefariki.
Msemaji wa UNHCR Italia, Bi. Carlotta Sami aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa boti mbili zilihusika katika ajali hiyo na zilikuwa zikitokea Libya huku kila moja ikiwa na zaidi ya watu 100.
Hakuna Stori itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook