Mwanasiasa wa Uganda ambaye pia alikuwa mgombea urais wa Chama cha Upinzani, Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine, amekamatwa katika mji Mkuu wa Kampala.
Taarifa zinasema wakati Bobi Wine anakamatwa, alikuwa anaongoza timu ya wabunge kutoka Chama chake cha National Unity Platform, kufanya maandamano dhidi ya kukamatwa na kutoweka kwa wafuasi wa chama chake katika kipindi cha kuelekea, wakati na baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Januari.
Vikosi vya usalama vilifyatua vitoza machozi na kutawanya waandamaji waliokuwa wameandamana na mwanasiasa huyo.
Inasemekana kwamba waliokamatwa ni pamoja na wabunge 15.
Katika mkutano uliofanyika kupitia njia ya video, Bobi Wine alitoa wito kwa wafuasi wake kutumia njia za amani kuandamana dhidi ya matokeo ya uchaguzi – ambayo anaendelea kudai kuwa vikosi vya usalama itoe wale wasiojulikana walipo.