Wakili wa mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda, Bobi Wine, amethibitisha kwamba mteja wake anatarajiwa kufanyiwa upasuaji, siku moja baada yake kujeruhiwa kwenye mguu wake.
Awali chama chake kilikuwa kimeripoti kwamba kiongozi huyo wa upinzani alipigiwa risasi kwenye mguu wake wakati wa mvutano kati yake na maofosa wa polisi.
Bobi Wine, 42, mkosoaji mkubwa wa rais wa Uganda Yoweri Museveni alikuwa katika mji wa Bulindo, karibia kilomita 20 kutoka jiji kuu la Kampala, wakati chama chake cha National Unity Platform (NUP) kiliripoti kutokea kwa tukio hilo.
George Musisi, wakili wa mwanasiasa huyo, ameiambia AFP kwamba mteja wake kwa sasa hayuko katika hali ya hatari ila kwa mujibu wa madaktari wake anahitaji kufanyiwa upasuaji ilikuondoa vipande vya bomu la machozi kutoka kwenye mwili wake.
Aidha wakili wake amedai kwamba polisi walikuwa wanamlenga kimakusudi mwanasiasa huyo wa upinzani.