Mmoja wa watu mashuhuri nchini Nigeria, mwanamke aliyebadili jinsia anayefahamika kwa jina la Bobrisky, aliyekamatwa kwa tuhuma za kutumia vibaya pesa amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela.
Bobrisky, ambaye jina lake halisi ni Idris Okuneye, anadaiwa kutumia vibaya na kukata noti za naira wakati wa onyesho la kwanza la filamu mjini Lagos, mamlaka iliambia BBC.
Wanasema “alimwaga” noti, kumaanisha kwamba alizirusha hewani kwa ishara ya kushukuru.
Mtindo wa “Kumwaga pesa” aina hiyo kwa kawaida hufanywa katika harusi na sherehe za Nigeria.
Hili kitaalamu ni kosa kwani noti huanguka chini ambapo zinaweza kukanyagwa.
Hajapewa chaguo la kulipa faini badala yake, ripoti ya vyombo vya habari vya ndani.