Bodi ya Filamu Tanzania imewasili Mkoani Geita na kukutana na wadau mbalimbali wa Filamu Mkoani Humo katika kukusanya Baadhi ya kazi ambazo wamekuwa wakizifanya kwa ajili ya kwenda kuzishindanisha katika Kilele cha tuzo za Filamu Tanzania 2022 zinazotarajiwa Kufanyika Jijini Arusha Desemba 18 Mwaka huu.
Akizungumza na Ayo TV Meneja Mipango na Masoko kutoka Bodi ya Filamu nchini Goodluck Chuwa amesema mpaka sasa wamekwisha kutembelea na kukusanya Filamu hizo katika mikoa 12 toka wameanza zoezi hilo huku akisema Bodi ya Filamu imeweka mikakati imara katika kusimamia kazi za wasanii wa Filamu hapa nchini.
“We fikiria Mwaka 2018 sekta ya Filamu ilikuwa kwa asilimia 13 na kwa taarifa yenu sasa Tanzania ni ya Pili kwa kuzalisha Filamu nyingi Barani Afrika ya kwanza ni Nigeria lakini ya Pili ni Tanzania, “- Chuwa.
Chuwa amesema takwimu ya mwaka 2018 inaonyesha kuwa Sekta ya Filamu nchini ilikuwa kwa Asilimia 18 huku ikishika nafasi ya pili Barani Afrika Chuwa amewataka vijana kuendelea kujituma katika kuweka ubunifu kwenye kazi .
Rosemary Poul ni Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji wa Filamu Mkoa wa Geita amesema wameishukuru Bodi ya Filamu nchini kwa kuona kilio cha waigizaji wa Mkoa wa Geita na kuwatembelea.
” Kwanza nipende kuwashukuru Bodi ya Filamu nchni kwa kuona mchango wetu waigizaji wa Filamu ndani ya Mkoa wa Geita kwa kuja kukagua na kuzichukua kwa ajili ya kwenda kuzishindanisha katika vipengele mbalimbali vya tuzo,” Bi.Rosemary.
Naye Sagali Mganga ni Muigizaji wa Filamu kutoka Mkoa wa Geita amesema ni hatua kubwa kwa waigizaji ndani ya mkoa wa Geita kuchangamkia fursa hii kwa waigizaji .