Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amewasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka 2023/2024 ambapo moja ya aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kwamba katika mwaka 2023/24, Bodi ya Michezo ya Kubahatisha inatarajia kutoa leseni 11,880 kwa Waendesha michezo ya kubahatisha, ambapo 2,273 ni leseni mpya na 9,607 ni leseni zitakazohuishwa.
“Katika mwaka 2022/23, Bodi
ya Michezo ya Kubahatisha ilitarajia kutoa leseni 7,697 kwa Waendesha michezo ya kubahatisha ambapo 1,923 ni leseni mpya na 5,774 ni leseni za kuhuishwa, kufanya ukaguzi kwa Waendesha michezo ya kubahatisha 83, kufanya mapitio ya Sheria na Kanuni za Michezo ya kubahatisha na kurejesha Bahati Nasibu ya Taifa”
“Hadi Aprili 2023, Bodi imetoa jumla ya leseni 8,778 sawa na asilimia 114 ambapo leseni mpya 3,658 na zilizohuishwa 5,120, kufanya kaguzi 88 sawa na asilimia 106, kuandaa mapendekezo ya mapitio ya Sheria na Kanuni za Michezo ya kubahatisha, uteuzi wa kampuni ya kuendesha Bahati Nasibu ya Taifa upo katika hatua za mwisho na unatarajiwa kukamilika Juni 2023 ambapo uendeshaji utaanza katika mwaka 2023/24”
“Katika mwaka 2023/24, Bodi ya Michezo ya Kubahatisha inatarajia kutoa leseni 11,880 kwa Waendesha michezo ya kubahatisha ambapo 2,273 ni leseni mpya na 9,607 ni leseni zitakazohuishwa, kufanya ukaguzi kwa Waendesha michezo ya kubahatisha 101 na kusimamia uendeshaji wa Bahati Nasibu ya Taifa”