Bodi ya utalii nchini TTB Imewaleta mawakala wa safari za watalii kutoka nchini Ujerumani na kuwakutanisha na Wadau wa biashara hiyo hasa ukanda wa kusini mwa Tanzania kwa lengo la kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana ukanda huu na kuongeza idadi ya wageni kuvitembelea .
Akiongea na AYO TV Hoza Mbura Afisa Utalii TTB kanda ya kusini amesema lengo la kuzidi kutangaza utalii wa kusini kama kitovu cha kutembelewa duniani kote kwanza ni kuhakikisha mawakala wanaofanya biashara hii wanavifahamu na kufanya kazi kwa pamoja na wadau wa biashara hizi ili kuleta wageni
Ayo Tv imeshuhudia mawakala hao kutoka nchini Ujerumani na wafanya biashara wenye makampuni ya kutembeza watalii nchini wakizungumza namna ya kushirikiana kuleta wageni.
Hata hivyo nao baadhi ya washiriki wa mkutano huo ulioandaliwa na bodi ya Utalii nchini TTB kwa ufadhili wa mradi wa kuboresha usimamizi wa maliasili na kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania REGROW Beatrice Massawe ameishukuru bodi ya utalii kwa kuwakutanisha na mawakala hao wa utalii kutoka Ujerumani
“ kiukweli tumeanza kupata mwanga mwingine na tunawakaribisha pia Watanzania watembelee vivutio hivi vya utalii kusini kwa sababu hawa mawakala wametoka Ujerumani kwaajili ya kuja kutusaidia sisi kututangasia nchi yetu hasa ukanda wa kusini “ Amesema Beatrice Massawe
Vilevile baadhi ya mawakala wa safari za watalii Nchini Ujerumani wamesema “ lengo la kutangaza ukanda wa utalii kusini mwa Tanzania ukiwa ujerumani ukanda huu wa kusini unafahamika sana na maeneo mengi watalii wameshatembelea kama hifadhi ya Taifa Ruaha na tumefurahishwa na uzuri wa eneo hilo hasa ukijani wa Asili “