BOHARI ya Dawa (MSD) imesema usambazaji wa dawa na vifaa vya kisasa Kisiwani Mafia mkoani Pwani imefanikiwa kupunguza rufaa za wagonjwa kutoka kisiwani humo kwenda kutibiwa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kisiwani Mafia Afisa Huduma kwa Wataeja wa MSD wa kanda hiyo Diana Kimario, alisema bohari hiyo imefanikiwa kupunguza rufaa za wagonjwa kutoka kisiwani Mafia kwenda jijini Dar es Salaam kwa kufunga vifaa tiba vya kisasa hususani vya maabara na upasuaji.
“Wilaya hii ina vituo vya afya 25 ambapo vituo 21 vipo Mafia na vituo vine vipo katika visiswa vidogo, ambapo vifaa vilivyosambazwa na MSD vitafanikisha kupunguza changamoto ya rufaa kwa wagonjwa waliokuwa wakisafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam kwa ajili ya huduma,”alisema.
Alisisitiza kuwa wamefanikiwa kusambaza Xray mashine, vitandaa vya kuchangia damu, mashine za kusaidia upumuaji, jenereta kubwa na ndogo na vifaa vingine vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 450,”alisema.
Diana alisema hatua hiyo imefikiwa kutokana na maboresho makubwa yaliyofanywa na Rais Dk.Samia kwa hospitali hiyo kuwa na majengo ya kisasa yanayokidhi vifaa vilivyofungwa hususani jengo la dharula na wagonjwa mahututi (ICU).
Alisema, pamoja na mafanikio hayo wamekuwa wakikutana na changamoto ya usafirishaji wa dawa na vifaa tiba kutokana na tozo wanazokutana nazo bandarini hivyo wanaiomba serikali kuona namna ya taasisi husika ikiwemo wilaya, MSD na bandari kukaa pamoja na kutoa msamaha kwa bidhaa za afya.
“Kuleta gari ya dawa na vifaa tiba Mafia ni gharama unalipia kivuko na kodi kwa bandari na Nyamisati na Mafia na iwapo tutashindwa kulipia inatulazimu kushusha mzigo na kupakia katika meli na wanapofika Mafia kutafuta gari ndogo za serikali au za kukodi kusambaza ambapo usambazaji unachukua muda mwingi.