Moja kati ya taarifa zilizokuwa zimewashitua wengi ni baada ya jina la Thomas Ulimwengu kujumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kwa ajili ya michezo ya kirafiki iliyopo katika kalenda ya FIFA dhidi ya Algeria na DRC Congo lakini wakihoji Ulimwengu ameitwa mbona hana timu kabla ya kugundulika kuwa anacheza FK Sloboda ya Bosnia.
Ulimwengu baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza jeraha lake la goti na kuachana na timu yake ya AFC Eskilstuna ya Sweden, wiki iliyopita aliripotiwa kuwa amejiunga na club ya FC Sloboda ya Bosnia lakini hakuwa amepata nafasi ya kuichezea kwa sababu ya kukosa vibali vya kufanyia kazi na kuishi.
Rais wa club ya FK Sloboda Feni Senad Mujkanovic amethibitisha kuwa Ulimwengu ana mchezaji mwenzake Rijeka Ivor Weitzer watakuwa huru kuichezea timu hiyo kuanzia weekend hii kwani vibali vyao vitakuwa vimepatikana rasmi, wakati huu timu yao ikijiandaa na mchezo dhidi ya Vitez.
“Kila kitu tulichotakiwa kukamilisha kwa upande wetu kimekamilika na kesho tunategemea vibali vya makazi na vibali vya kazi vya hawa wachezaji wawili (Ulimwengu na Weitzer) vitapatikana, naamini wote watapatika kuanzia michezo ya weekend ijayo”>>>>> Feni Senad Mujkanovic
CHANZO: tuzlalive.ba
Alichozungumza Makamu wa Rais wa TFF baada ya kufungiwa maisha