Shambulizi la bomu la kujitoa mhanga, limetokea kaskazini mwa Nigeria katika eneo la Yobe ndani ya ukumbi ambao mashabiki walikuwa wamejaza kutazama mechi za kombe la dunia.
Hali ya tahadhari ilitangazwa katika majimbo matatu ikiwa ni pamoja na Yobe huku washukiwa wa mashambulizi hayo wakiwa ni kundi la wanamgambo wa Boko Haram.
Mashuhuda wa tukio hilo wanasema mshambuliaji wa kujitoa mhanga alikuwa ndani ya gari ndogo iliyokuwa imetegwa bomu wakati watu wakiangalia mechi kati ya Brazil dhidi ya Mexico Jumanne jioni.
Ukumbi ambao mashambulizi yamefanyika ni maarufu sana na mara nyingi watu wengi hupenda kwenda kuangalia matukio makubwa.
Hata hivyo, mamlaka nchini Nigeria ilitoa onyo kwa wakazi katika baadhi ya maeneo kuepuka kukaa sehemu za mkusanyiko kipindi hiki cha kombe la Dunia wakiogopa mashambulizi ya wapiganaji.
Wachambuzi wanasema kuwa vikundi vya wapiganaji wa Kiislam, ikiwa ni pamoja na Boko Haram, wameelezea mpira wa miguu kama kitu kisichofaa katika dini ya Kiislamu.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta FB