Mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast anayeichezea klabu ya Manchester City ya Uingereza Wilfried Bony August 28 amepost picha katika mtandao wa Instagram inayomuonesha akiwa anatembelea magongo huku mguu wake ukiwa umevalishwa kiatu maalum cha plastic kwa ajili ya majeraha aliyoyapata katika mguu wake wa kushoto.
Wilfred Bony alijiunga na klabu ya Manchester City akitokea klabu ya Swansea City kwa ada ya uhamisho ya pound milioni 28. Kocha wa klabu ya Man City Manuel Pellegrini amethibitisha kumkosa mchezaji huyo katika mechi ya kesho dhidi ya Watford.
“Kwa bahati mbaya Bony alipata majeraha jana hivyo hatokuwepo katika mchezo wa kesho na huenda akawa nje ya uwanja kwa siku saba hadi kumi”>>> Manuel Pellegrini
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos