Kocha wa Manchester United Ruben Amorim anadai kufurahishwa na kile anachokiona kutoka kwa Antony.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil amezoea nafasi mpya ya beki wa pembeni chini ya Amorim tangu kuwasili kwa Mreno huyo.
Meneja huyo aliiambia talkSPORT baada ya ushindi dhidi ya Manchester City: “Nafikiri, tulipoanza, kila mtu ni tokea mwanzo.
“Tulichukua kama mwezi mmoja kueleza kuwa kila kitu kina mwanzo mpya kwa sababu kila mtu anastahili mwanzo mpya na nguvu iko mikononi mwake kwa sababu wakionyesha nitawaweka wacheze.
“Nataka tu kushinda. Wanawajibika kucheza, sio mimi.
“Alifanya kazi kubwa kuimarika katika nafasi hiyo. Anatakiwa kujilinda zaidi lakini ana uwezo wa kuifanya na anatakiwa kufanya hivyo mwenyewe.”