Mega Beverages Limited (MBL), Kampuni
inayotambulika katika sekta ya vinywaji Tanzania, imeadhimisha miongo miwili ya mafanikio kwa kuzindua toleo maalum la K-Vant Premium Spirit.
Bidhaa hii ya toleo maalum, itapatikana kwa muda mfupi tu hadi shehena itakapomalizika, inakuja kwa wakati muafaka wa msimu huu wa sikukuu,
ikiahidi kuleta shangwe kupitia kinywaji chake cha kipekee ambacho kimetengenezwa na magalighafi ya hapa nchini.
Toleo hili maalum, ambalo ni la kwanza na la aina yake nchini Tanzania, linaakisi shamrashamra za msimu wa sikukuu katika kuleta watu pamoja,
kushukuru na kufurahi. Toleo hili linajivunia kuwa na chupa ya kisasa na rangi ya dhahabu, K-Vant Premium Spirit Special Edition imewekwa mahsusi kama zawadi ya kipekee inayochanganya ustadi wa hali ya juu na umuhimu wa tukio husika.
Hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika Dar es Salaam ilijumuisha mchanganyiko wa kumbukumbu na matarajio, ambapo wadau mbalimbali walitoa pongezi kwa mafanikio ya chapa hiyo. Mgeni Rasmi, Bw. Gilead Teri, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), aliisifu Mega Beverages kwa umakini wake katika kutengeneza bidhaa zenye ubora na matumizi ya malighafi za ndani.
“K-Vant Special Edition ni Ushuhuda wa ari ya ujasiri na ubunifu wa Mega Beverages,” alisema Teri. “Toleo hili maalum si tu linaonyesha dhamira yake ya
utengenezaji wa bidhaa bora, bali pia linaonyesha nguvu na uwezo mkubwa wa uzalishaji wa ndani na mchango wake kwa uchumi wetu.
Christopher Ndosi, Meneja Mkuu wa Mega Beverages, alizungumza kuhusu hatua zilizopigwa na kampuni hiyo, akisema: “Hii ni zaidi ya shamrashamra; ni
ahadi kwa wateja wetu. ‘K-Vant Special Edition’ inawakilisha ubora wa hali ya juu na maadili ya kibunifu ambayo yana mchango mkubwa kwenye safari yetu.
Ikitengenezwa kwa malighafi ya asili ya hapa nchini, ni heshima kwa urithi wetu na matukio ya kumbukumbu tunayolenga kuyatengeneza.”
Kwa upande wake, Narcisius Ngaillo, Meneja wa Mauzo na Usambazaji, alielezea juhudi kubwa zilizofanywa kuhakikisha bidhaa hii inapatikana kwa
urahisi:
“Tunahakikisha kwamba Watanzania kote nchini wanapata nafasi ya kufurahia au kutoa zawadi ya kinywaji hiki chenye ubunifu wa hali ya juu. Yote ni katika kuhakikisha msimu huu wa sikukuu kuwa wakipekee zaidi.
Meneja wa Chapa, Awatif Bushiri, alichangia maoni sawa na hayo alisema “K-Vant Special Edition imehamasishwa na watanzania na uthubutu wao wa
kila siku na ari ya kutokata tamaa katika kufanikisha kesho iliyo bora.
Tunakaribisha kila mtu kufurahia na kushiriki kitu cha kipekee kabisa.” Bushiri alisisitiza upekee wa bidhaa hiyo, akibainisha mvuto wake kama zawadi
ya msimu wa sikukuu: pombe kali yenye rangi ya dhahabu, inayounganisha ladha za mimea safi na harufu inayovutia.
Katika kuangazia siku zijazo, Mega Beverages inatarajia kuendelea kupanua soko lake nchini na nje ya Tanzania. Kama sehemu ya mkakati wake wa ukuaji, Kampuni inapanga kuanzisha bidhaa mpya za kibunifu zinazolingana na ladha pendwa kwa wateja ambazo zinabadilika mara kwa mara huku zikizingatia
utamaduni wa hapa nchini.
“Mipango yetu ya kukuza bihashara ni endelevu kwa manufaa ya wengi kupitia bidhaa tulizozianzisha huku tukiendana na fursa mpya,” alisema Ndosi
“Mustakabali wa Mega Beverages ni mzuri, na yajayo yanafurahisha. Kadri msimu wa sikukuu unavyoendelea, toleo hili maalum la K-Vant Special
Edition linatoa njia ya kipekee ya kusherehekea mafanikio ya maisha kwa ladha ya dhahabu. Cheers Kwetu Sote.