Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imewataka wamiliki wa hoteli za nyota tatu hadi tano nchini kuhakikisha hadi ifikapo Julai Mosi mwaka huu wawe wameshakata leseni ya kumiliki na kuendesha maduka ya kubadilishia fedha za kigengi kwenye hoteli zao.
Hayo yalibainishwa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutuba wakati wa kikao maalumu na wamiliki wa hoteli jijini Arusha jana kwa lengo la kupokea maoni yao kuhusu maduka hayo.
Tutuba alisema sekta ya hoteli ni wadau muhimu kwa uchumi wa nchi kwa kuwa ni sekta iliyoungana na sekta ya utalii kwa kuwapokea, kuwahifadhi na kuwahudumia watalii.
Alisema kwa kuwa baadhi ya watalii hufika kwenye hoteli hizo nyakati za usiku au nyakati za sikukuu hali inayowafanya washindwe kupata huduma ya kubadilisha fedha za kigeni walizonazo, hivyo amesema BoT imeamua kubadilisha kanuni zake kwa kuruhusu wamiliki wa hoteli hizo kuwa na maduka ya kubadilishia fedha za kigeni kwa ajili ya wageni wanaowapokea.
Mwenyekiti wa Chama cha wakala wa Utalii Tanzania Wilbard Chambulo amesema benki kuu inatakiwa kupitia upya utaratibu huo ikiwemo mgeni kutokulipa kwa fedha taslimu pamoja nakutumia card au kutumia mifumo ya kibenki