October 28 2016 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Benno Ndullu aliita waandishi wa habari kwa Dharura, mbele ya waandishi wa Habari Benno Ndullu ametoa taarifa kuwa Benki kuu ya Tanzania imechukua usimamizi wa benki ya Twiga ‘Twiga Bancorp’ kuanzia October 28 2016.
Gavana wa benki hiyo ameeleza kuwa uamuzi huo umechukuliwa baada ya kubaini kuwa benki ya Twiga ina upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na matakwa ya sheria ya mabenki na taasisi za fedha ya mwaka 2006 na kanuni zake.
Upungufu huu wa mtaji umeelezwa unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na pia kuendelea kutoa huduma za kibenki kwa benki ya Twiga kutahatarisha usalama wa amana za wateja wake.
Kutokana na uamuzi huo benki kuu ya Tanzania imesimamisha bodi ya wakurugenzi na uongozi wa benki ya Twiga na imemteua Meneja msimamizi ambaye atakuwa na jukumu la kusimamia shughuli za benki ya Twiga kwa kipindi ambacho itakuwa chini ya usimamizi wa benki kuu.
BoT imesema kuwa katika kipindi kinachokadiriwa kufikia wiki moja kuanzia siku leo October 28 2016, shughuli za utoaji wa huduma kibenki za benki ya Twiga zitasimama ili kutoa nafasi kwa ajili ya kupanga taratibu za uendeshaji wa benki hiyo.
UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
ULIKOSA MATUKIO SITA YA UDANGANYIFU YAIYOTOKEA KATIKA MTIHANI WA DARASA LA SABA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI