Zikiwa zimebaki siku 29 kabla ya kuanza kwa michuano ya kombe la dunia mwaka 2014 kuanza, usalama bado umeonekana kuwa tatizo nchini humo manake mapema wiki hii kwenye mitandao tofauti nchini humo imeonekana video moja ikionyesha mchezo wa timu za mchangani, ambapo adhabu ya penati iliyotolewa na mwamuzi ilisababisha vurugu zilizohusisha silaha kali kama bunduki AK-47 na risasi kupigwa.
Watu kadhaa waliokuwa wamevalia jezi za timu ya taifa ya Brazil wakiwa na silaha zao walianza kurusha risasi juu kwa muda usiopungua sekunde 35.
Tukio hilo lilitokea kwenye eneo la Bangu, magharibi mwa mji wa Rio de Janeiro kwenye nchi ya Brazil ambayo unaambiwa kila mwaka watu karibu elfu sitini huuwawa kwenye visa vya silaha kama hizi.
Unapenda chochote kinachonifikia kisikupite? jiunge na mimi twitter kwa kubonyeza HAPA pia facebook na Instagram kwa kubonyeza FB na INSTA ili nikutumie kila kitu, kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi.