Kama hujawahi kusafiri kwenda mikoa ya kusini naomba nikusafirishe kwa picha hizi ambazo zinaonyesha hali ya kipande kibovu kinachowakalisha muda mwingine kwa zaidi ya saa 10 wasafiri wa mikoa ya kusini hasa inaponyesha mvua.
Kuna kipindi bidhaa hupanda hasa kwa sehemu kama Lindi, Mtwara, Masasi, Nachingwea, Newala, Tandahimba na baadhi ya sehemu ambazo hutegemea barabara hii kusafirishia bidhaa na abiria.