Hatimaye kile ambacho kilikua kinasubiriwa kwa hamu kimepata majibu, ni mchakato wa kumpata Mgombea Urais Zanzibar kwa ticket ya Chama cha Mapinduzi CCM katika Uchaguzi Mkuu wa October 2020.
Taarifa ikufikie kwamba Chama cha Mapinduzi (CCM) kimempitisha Dr. Hussein Mwinyi kuwa Mgombea Urais wa CCM Zanzibar baada ya kupata kura 129 sawa na asilimia 78.65 ya kura zote zilizopigwa ambapo Dr. Mwinyi kabla ya kutangazwa Mshindi alikua amebaki kwenye tatu bora akiwa na Dkt. Khalid Salum Mohamed na Shamsi Vuai Nahodha.
Kabla ya Dr. Mwinyi kutangazwa Mshindi, Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa CCM alisema “Wote hawa watatu ambao tutawapigia kura ili kumpata mmoja wanafaa ila yupo mmoja anayefaa zaidi ni jukumu lenu kumchagua anayefaa na nina matumaini kati ya hawa mmoja atakuwa Rais wa Zanzibar”
“Tusichukiane, mimi niliomba kura na Mzee Pinda na nikampindua, Makongoro Nyerere na wengine ila leo tupo hapa,kazi hizi ni za kupita, wagombea wote 31 nawapongeza kwa kuchukua fomu atakayepita mmoja tumuunge mkono, saa nyingine maneno yanaletwa na upinzani na CCM tunayabeba”- Rais Magufuli.
MAAJABU: DUKA LISILO NA MLANGO WA MBAO WALA WA CHUMA NA HAKUNA ANAYETHUBUTU KUDOKOA HATA KIBERITI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA MWANZO MWISHO
EXCLUSIVE: DODOMA KAMA ULAYA STAND MPYA YA MABASI NI KAMA AIRPORT, YASHIKA NAMBA 1 TANZANIA NZIMA, INA KANISA NA MSIKITI NDANI