Leo February 24, 2020 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuhukumu Mwandishi wa Habari, Erick Kabendera kulipa fidia na faini ya Sh.Mil 273 baada ya kukiri makosa yake ya utakatishaji fedha na kukwepa kodi.
Pia mahakama hiyo imemuhukumu kulipa faini ya Sh.250,000 (Laki Mbili na Elfu hamsini) ama kwenda jela miezi 3 baada ya kukiri kosa la kukwepa kodi.
Hukumu imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega baada ya Kabendera kusota korokoroni kwa miezi 6 tangu alipofikishwa mahakamani hapo Agosti 5, 2019.
Kabendera anatakiwa kulipa kiasi cha Sh.Mil 173 ndani ya miezi 6, huku kiasi cha Sh.Mil 100 akiwa tayari ameshaingiza katika akaunti ya Serikali.
Kabendera kwa sasa yupo huru, huku akitakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha.
Katika kesi hiyo, Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa Sh.Mil 173.
Inadaiwa kuwa katika kipindi hicho, Kabendera alijihusisha na mtandao wa kihalifu kwa kutoa msaada kwa genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.
Inadaiwa kuwa katika kipindi hicho, bila ya sababu alikwepa kodi ya Sh.Mil 173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Pia inadaiwa Kabendera alitakatisha Sh. 173,247047.02 huku akijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la kujihusisha na genge la uhalifu na ukwepaji kodi.
KAMANDA AMJIBU HARMONIZE “NI MKOSAJI, WAZIBE MDOMO HUYO NI MUONGO, USHAHIDI UPO”