Sriwijaya Air, Ndege ya Abiria ya Indonesia ambayo iliripotiwa kupoteza mawasiliano muda mfupi baada ya kupaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Jakarta, imeanguka ikiwa na abiria 62, Wizara ya Usafirishaji ya Nchi Indonesia imethibitisha.
Awali mashuhuda walisema wameiona Ndege ikilipuka karibu na Kisiwa cha Pulau Laki Nchini Indonesia.
Taarifa hizi zinakuja saa kadhaa tangu ripoti ya Sriwijaya Air, Ndege ya Abiria ya Indonesia kupoteza mawasiliano muda mfupi baada ya kupaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Jakarta, Ndege hiyo ya SJ182 Boeing 737-500 inatajwa kuwa na miaka 26 ya kazi.
CGTN wanaripoti kuwa tayari Meli ya utafutaji na uokoaji imetumwa eneo hilo ambako inaaminika Ndege hiyo ilielekea baada ya kupoteza mawasiliano.