Siku ya mwisho ya usajili barani ulaya imefungwa kwa staili ya aina yake na klabu ya Manchester United baada ya kufanikiwa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia Radamel Falcao.
United ambao leo hii imewauza washambuliaji wake wawili Chicharito na Danny Welbeck – imethibitisha kumsajili Falcao kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa mkopo huku wakiwa na option ya kumnunua moja kwa moja msimu ujao.
Falcao anakuwa mchezaji wa sita kujiunga na Man United wakati wa dirisha hili la usajili, baada ya Luke Shaw, Herrera, Blind, Di Maria, na Rojo.
Kocha Louis Van Gaal amesema mchezaji wa aina ya Falcao anakupokuwa na uwezekano wa kumpata basi hiyo sio nafasi ya kuipoteza.
Falcao nae alisema: “Nina furaha kujiunga na Manchester United kwa mkopo. Manchester United ni klabu kubwa zaidi duniani na ina kila sababu ya kurudi kuwa juu tena. Nipo tayari kufanya kazi na Louis van Gaal na kuisadia timu kupata mafanikio katika kipindi nitakachokuwepo kwenye klabu.”