Saa kadhaa baada ya club ya Tottenham Hotspurs kutangaza kumfuta kazi rasmi aliyekuwa kocha mkuu wa club hiyo Mauricio Pochettino, leo imefikia maamuzi na kuingia mkataba na kocha wa zamani wa Man United na Chelsea Jose Mourinho.
Tottenham chini ya mwenyekiti wao Daniel Levy wametangaza kuingia mkataba wa miaka mitatu na Jose Mourinho wa kuifundisha timu yao ambayo msimu huu imekuwa ikisuasua, Mourinho sasa atakuwa kocha wa Tottenham Hotspurs hadi 2023.
“Kwa Jose (Mourinho) tunae mmoja kati ya makocha waliowahi kufanikiwa katika soka, ana utajiri wa uzoezu na anaweza kuihamasisha timu na mtaalam mkubwa wa mbinu, ameshinda mataji katika kila club aliyowahi kufundisha” >>> Daniel Levy
Mourinho anajiunga na Chelsea akiwa na kumbukumbu ya kushinda mataji ya matatu ya EPL akiwa na Chelsea, huku akiwa na rekodi ya kuwa mwa makocha wa tatu pekee waliowahi kutwaa UEFA Champions League wakiwa na club mbili tofauti (FC Porto 2004, Inter Milan 2010), Mourinho anaichukua Spurs ikiwa nafasi ya 14 katika Ligi huu kutoka kufika fainali ya UEFA Champions League msimu uliopita (2018/2019).
VIDEO: BONDIA ARNEL TINAMPAY NAMBA 2 KWA UBORA PHILIPINE BAADA YA MANNY PACQUIAO KATUA DSM