Wanafunzi wa Kitanzania ambao walikwama Sumy nchini Ukraine wakiwa pamoja na Wanafunzi wengine wa Mataifa mbalimbali wanaosoma Sumy State University wamefuatwa muda huu na magari ya msalaba mwekundu tayari kuwatoa Sumy na kuwasafirisha hadi Jiji la Poltava nchini Ukraine ambako huko watachukua Treni kwenda Jiji la Lviv, Ukraine ambako ni Mpaka kati ya Ukraine na Poland au wanaweza kwenda Hungary.
Mapema leo kundi la wanafunzi 11 waliokuwa wamekwama Sumy nchini Ukraine wameoneka katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Urusi Balozi Frederick Kibuta na Maafisa Ubalozi baada ya kuwasili Moscow nchini Urusi salama na hawa ni Wanafunzi ambao walifanikiwa kuvuka hadi Urusi.
Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, Vassily Nebenzia, amesema Nchi yake imesitisha mapigano kuanzia saa nne asubuhi ya leo kwa majira ya Moscow na kufungua njia salama kuwahamisha Raia kutoka miji ya Kiev, Cher-nigov, Sumy na Mariupol nchini Ukraine.
WANAUME NCHINI UKRAINE IMEBAINIKA KUJIFICHA KWENYE MAGARI “WATOROKA WASISHIRIKI VITA”