Kufuatia kupotea kwa chombo cha majini cha ‘Titan’ Kampuni ya OceanGate imethibitisha mapema hii leo kwamba inaamini kuwa abiria wa submarine hiyo iliyozama chini ya maji kwa dhumuni ya abiria watano waliokuwemo kutazama mabaki ya meli ya Titanic, wamepoteza maisha.
Mkuu wa Walinzi wa Pwani kutokea Marekani amesema “Sasa tunaamini Mkurugenzi Mtendaji wa Oceangate, Stockton Rush, Shahzada Dawood akiwa na Mwanae Suleman Dawood, Hamish Harding pamoja na Paul-Henri Nargeolet, wamepotea kwa huzuni”
“Wanaume hawa walikuwa Wagunduzi hodari walioshiriki kufanya zoezi hilo kubwa kwa dhumuni la kulinda bahari za ulimwenguni, mioyo yetu iko pamoja na roho hizi tano na kila Mwanafamilia katika kipindi hiki cha maombolezo, tunahuzunika kuwapoteza Watu hawa pamoja na furaha waliyoleta kwa kila Mtu waliyemjua”