Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania imeiambia millardayo.com na AyoTV kwamba tetemeko la ardhi lililotokea leo kanda ya ziwa kwenye miji kama Bukoba limesababisha madhara makubwa na watu wengine wamepoteza maisha.
Mamlaka hiyo imesema japo mpaka sasa haijapata idadi kamili ya waliojeruhiwa, idadi ya waliofariki kutokana na tetemeko hilo mpaka jioni ya leo September 10 2016 ni Watanzania wanne ambapo bado juhudi za uokoaji zinaendelea kufanyika.
AyoTV na millardayo.com zinaendelea kufatilia taarifa zaidi na utaendelea kuzipata kadri zinanifikia lakini kama unahitaji maelezo ya awali ya Mwandishi wa habari ambaye ni shuhuda wa tetemeko la leo Bukoba, bonyeza play hapa chini.