Wakati Watanzania wakiendelea kupaza kilio chao, kutapeliwa fedha zao na Kampuni ya Kalynda E-Commerce Limited inayojishughulisha na biashara mandao, Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imesema kampuni ilipewa leseni ya uuzaji wa jumla wa vifaa vya kielectroniki na mawasiliano kwa nia mtandao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Oktoba 12, Mwaka huu, Brela imekiri kuifahamu kampuni hiyo lakini kufanya biashara ya Upatu “Pyramid Business” ya kukusanya fedha kutoka kwa wananchi kwa ahadi ya kupata faida ndani ya muda fulani ni kinvume na bidhaa au huduma ilivoombewa na kupata leseni.
“Kampuni ya Kalynda E-Commerce Limited ilisajiliwa tarehe 14 Juni, 2022 na kupewa cheti cha usajili Namba. 156483877. Kwa mujibu wa katiba ya kampuni (Memorandum and Articles of Association) shughuli kuu za kampuni ni pamoja na uuzaji wa jumla wa vifaa vya kielectroniki na mawasiliano, ufanyaji wa biashara ya kitekinolojia ya kimataifa mtandaoni,”‘ imesema Taarifa hiyo ilitolewa na Brela kupitia kitengo cha mawasiliano kwa umma imesema “wakati wa uwasilishaii wa maombi ya usajili wa Kampuni na Leseni ya Biashara taarifa zilizowasilishwa zilionesha ofisi ya Kalynda E- Commerce Limited zipo Kiwanja Na. 9, Mtaa wa Kaunda, Kata ya Msasani Wilaya ya Kinondoni, Dares Salaam,