YVONNE MASSELE ni msajili Msaidizi kutoka Wakala WA usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) amewatoa hofu vijana na wanawake kuhusu kusajili kampuni zao na Usajili wa jina kampuni ili wasikose fursa ya kutambulika kisheria katika biashara zao kitaifa na kimataifa.
Amesema hayo wakati wakitoa elimu ya Usajili wa kampuni na majina ya Leseni ya biashara kwa wateja waliofika kwenye Banda lao katika maonyesho ya wajasiliamali na Wafanyabiashara katika Viwanja vya mlimani city jijini Dar es salaam.
Alisema BRELA hutoka huduma za Usajili wa kampuni na Usajili wa jina la kampuni bure hivyo wafike katika Banda la maonyesho la hapo mlimani city au waingie kwenye mtandao wajisajili wenyewe popote walipo.
“Kuna fursa ambazo Mfanyabiashara anapata iwapo amesajili kampuni yake BRELA na hukosa fursa hizo iwapo hawajasaji Kampuni zao BRELA”
Aidha alizitaja fursa hizo kuwa ni pamoja na kupata tenda kubwa za kiserikali, unakuwa unatambulika kisheria lakini pia inaongeza sifa ya kupata Mikopo katika taasisi mbalimbali za fedha.
NICOLAS MASANJA pamoja na wameshukuru Kwa Elimu hiyo kuwataka watu wote kufanya hima kusajili kampuni zao hata kama wana wazo ambalo ni muhimu ili kuwa na hatimiliki ya ubunifu wa biashara zao.
Kundi hilo la Vijana na wanawake limepata faida ya kujua misingi ya kuanzisha kampuni Kwa kusajiliwa kwani wengi wao wanafanya biashara katika bila kufanya usajili na hivyo inawanyima fursa ya kutambulika kisheria.