Iran na Saudi Arabia ni miongoni mwa mataifa sita yaliyoalikwa Alhamisi kujiunga na kambi ya Brics ya nchi zinazoendelea kiuchumi. Umoja wa Falme za Kiarabu, Argentina, Misri na Ethiopia pia zinatazamiwa kujiunga na umoja huo kuanzia 2024.
Nchi nyingine zikiwa ni Argentina, Misri, Ethiopia, na Umoja wa Falme za Kiarabu zikuwa zitajiunga na Brics kuanzia Januari 1 mwaka ujao, rais wa Afrika Kusini amesema.
Tangazo hilo lilitolewa kwenye mkutano wa kilele wa Brics mjini Johannesburg na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, ambaye nchi yake ndiyo mwenyekiti wa sasa wa Brics.
BRICS kwa sasa inaundwa na nchi zinazoibukia kiuchumi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini. Wanachama hao watano walikubali katika mkutano wa kilele wa wiki hii kupanua kambi hiyo.
Ni mara ya pili kwa BRICS kuamua kujitanua ili kupata ushawishi zaidi duniani..
Umoja huo uliundwa mwaka 2009 na Brazil, Russia, India na China huku Afrika Kusini ikiongezwa mwaka wa 2010.
Kambi ya Brics inawakilisha karibu 40% ya watu duniani na inachangia zaidi ya robo ya Pato la Taifa la kimataifa.