Tumezoea kuona harusi nyingi wasichana ambao hufahamika zaidi kama wapambe au ‘Maids’ ndio hupewa jukumu la kusimama mbele na maharusi kwa lengo la kunogesha sherehe.
Lakini hii iko tofauti, imenivutia kumwona bibi nae yumo kwenye kwenye list ya wasimamizi !! bibi harusi Christine kamchagua bibi yake Nana Beth mwenye umri wa miaka 89 kumsimamia kwenye harusi yake pamoja na wasichana wengine.
Si ndugu zake tu walioshangazwa na uamuzi huo, bibi mwenyewe alishangaa kuona mjukuu wake anampa jukumu hilo, unaambiwa alimuuliza mjukuu wake zaidi ya mara 10 kama ana uhakika na anachokisema, jibu lilikuwa lilelile la kwanza !!
Wageni waalikwa walionesha kufurahia pia kumuona bibi nae yumo na hakuna kitu kilichomshinda wala kuonekana kigumu kwake mwanzo mpaka mwisho, hata kucheza pia.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos