Leo March 26, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya Iringa imemuachia kwa dhamana Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania Abdul Nondo ambaye alikuwa anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Iringa.
Hakimu mkazi mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, John Mpitanjia amesema dhamana ipo wazi na Nondo anatakiwa kudhaminiwa na watu wawili ambao ni wakazi wa Iringa, mmoja awe mfanyakazi wa Serikali, na wanatakiwa waweke bondi ya shilingi milioni 5 pamoja na kuwa na mali isiyohamishika.
Wakili wake, Jebra Kambole anashughulikia dhamana ya mwanafunzi huyo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Nondo anatuhumiwa kwa makosa mawili. Kosa la kwanza ni kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni March 7, 2018 akiwa Ubungo na kusambaza kwa kutumia mtandao wa WhatsApp kuwa yupo hatarini.
Shtaka la pili ni kutoa taarifa za uongo kwa watumishi wa umma mjini Mafinga alipokuwa akitoa taarifa katika kituo cha Polisi Mafinga kuwa alitekwa na watu wasiojulikana jijini Dar es Salaam na kupelekwa Kiwanda cha Pareto cha Mafinga.
#BREAKING Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa imemuachia kwa dhamana Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania Abdul Nondo
Masharti ya dhamana aliyopewa ni wadhamini wawili mmoja mtumishi wa Serikali wote wakazi wa Iringa na bondi ya kauli Tshs Mil 5, atarudi Mahakamani April 10 pic.twitter.com/TFbvxnLBrt
— millardayo (@millardayo_) March 26, 2018
LIVE: JPM kwenye uzinduzi wa magari 181 MSD ya kusambaza Dawa na Vifaa Tiba