Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo March 14, 2018 ameweka jiwe la msingi katika sehemu ya pili ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani “Standard Gauge” inayoanzia Morogoro hadi Makutupora Mkoani Dodoma.
Akiongea na wananchi na viongozi katika hafla hiyo JPM amewata Watanzania kufanya kazi kwa bidii ili kuacha kulalamika vyuma vimekaza.
“Asiefanya kazi asile, asipo kula afe, hiyo ndiyo lugha ya kuwaambia ukweli, mtu kama hafanyi kazi halafu analalamika vyuma vimebana amevibana mwenyewe” -Rais Magufuli#MillardAyoUPDATES
— millardayo (@millardayo_) March 14, 2018
“Asiyefanya kazi na asile na asipokula afe” -Rais Magufuli#MillardAyoUPDATES
— millardayo (@millardayo_) March 14, 2018