Umoja wa Ulaya upongeza serikali ya Burundi kwa kuwaacha huru wafungwa wapatao 740 waliokuwa wamekamatwa tangu mwaka 2015 kufuatia ghasia na vurugu zilizosababishwa na maandamano na jaribio la mapinduzi.
Mjumbe maalumu wa Umoja wa Ulaya nchini Burundi amepongeza uamuzi wa wizara ya sheria nchini humo kwa kuwaacha huru wafungwa 740 waliokuwa wamekamtwa katika matukio tofauti kufuatia jaribio la mapinduzi. Miongoni mwa watu walioachiwa huru, 450 walihusika na matukio ya mwaka 2015.
Taarifa hiyo ilitolewa katika tovuti ya Umoja wa Ulaya na kuomba vijana wachwe huru vijana wote waliokamatwa katika maandamano ya mwaka 2015.