LeBron James aliwashukuru mashabiki kwa upendo wao na maombi kwa ajili ya mwanawe Bronny, ambaye aliruhusiwa kutoka hospitali siku ya Alhamisi baada ya kupata mshtuko wa moyo alipokuwa akifanya mazoezi na timu ya mpira wa vikapu ya Chuo Kikuu cha Southern California (USC).
Mtoto huyo wa kiume mwenye umri wa miaka 18 wa mfungaji bora wa muda wote wa NBA alipatwa na mshtuko wa moyo siku ya Jumatatu na kukimbizwa katika Kituo cha Matibabu cha Cedars-Sinai ambako alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Kituo cha Matibabu cha Cedars-Sinai kilisema katika taarifa siku ya Alhamisi kwamba James alikuwa ameruhusiwa na alikuwa amerejea nyumbani akipumzika na familia yake.
“Nataka kuwashukuru watu wengi wanaotuma meneno ya upendo na maombi ya familia yangu,” alichapisha James kwenye jukwaa twitter, .