Mwigizaji maarufu wa Marekani Bruce Willis atapumzika kufanya kazi yake ya uigizaji kutokana na tatizo la kiafya linalosababisha uwezo wake wa kiakili uathirike, familia yake imesema.
Mtoto wake wa kike aitwae Rumer amepost Instagram na kusema “Kwa wafuasi wa Bruce, kama familia tulitaka kuwajulisha kwamba mpendwa wetu Bruce amekuwa akikabiliwa na matatizo fulani ya afya na hivi majuzi aligunduliwa na aphasia ambayo inaathiri uwezo wake wa kiakili.”
“Kutokana na hili na kwa kuzingatia sana Bruce anaachana na kazi ambayo imekuwa na maana kubwa kwake, huu ni wakati mgumu sana kwa familia yetu na tunathamini sana upendo wenu na support yenu” ——— Rumer.
Inaelezwa kwamba aphasia ni hali inayompotezea Mtu uwezo wa kuwasiliana na inaweza kusababishwa na kiharusi, jeraha la kichwa, uvimbe wa ubongo au ugonjwa.