Siku ya March 17, 2018 Serikali ya Urusi ilitangaza kuwafukuza wanadiplomasia 23 wa Uingereza ambao walikuwa wakifanya kazi nchini humo, hii ilikuwa ni baada ya Uingereza pia kufukuza wanadiplomasia 23 wa Urusi waliokuwa nchi Uingereza.
Hii ni kutokana na Mpelelezi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal alikutwa na mwanaye Yulia kupewa sumu na watu wasiojulikana wakiwa nyumbani kwao Uingereza, na serikali ya nchi hiyo kuituhumu Urusi kuhusika na tukio hilo.
March 20, 2018 jumla ya Warusi 80 ikiwa ni pamoja na wanadiplomasia 23 wamefungasha mizigo yao na kurudi kwao Urusi, baada ya kuambiwa mwisho wa kuwepo nchini humo ni wiki hii.
Tayari mabasi ya kubeba wanadiplomasia hao pamoja na familia yao yameonekana kuanza kuwaondoa watendaji hao wanaoishi Kensington, London.
“Yeyote atakayecheza na Mtoto wa kike, hatakuwa salama” – MWENYEKITI CCM