Leo June 28, 2018 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Kinondoni imesema idara zinazoongoza kulalamikiwa kwa vitendo vya rushwa ni TAMISEMI.
Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Kinondoni
Eugenius Hazinamwisho amesema kwa kipindi cha miezi 12 kuanzia July 2017 hadi June 2018 wameweza kupokea taarifa mpya, kufungua kesi mpya na kuendesha majalada yaliyopita.
Hazinamwisho amesema wamepokea taarifa 376 kutoka kwa wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari, ulinzi na usalama, idara na taasisi za umma na binafsi.
“Katika taarifa hizo idara zilizoongoza kulalamikiwa dhidi ya rushwa ni TAMISEMI ambapo taarifa 108 sawa na asumimos 28.72,” amesema Hazinamwisho
Katika taarifa hizo, asilimia 11.70 ni Polisi, sekta binafsi 10.37%, mahakamani 7.71%, ardhi 5.85%, na sekta ya elimu ni 3.72%.
“Katika taarifa hizo rushwa inayoongoza ni ile ya kuomba na kutoa, ambapo pia katika kipindi hiki cha July 2017 hadi June 2018 tumedhibiti na kuokoa jumla ya Sh.Mil 78.5,” Hazinamwisho
Hazinamwisho amewataka wananchi wote kuendelea kushirikiana na taasisi hiyo katika mapambano dhidi ya rushwa.
Rais Magufuli alivyompokea Rais wa Zimbabwe Mnangagwa