Mbunge wa Viti Maalum, Ester Bulaya, ametoa wito kwa Serikali kutoa mafunzo ya kutumia silaha kwa Vijana wachache wanaoshiriki mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) badala ya kuwafundisha wengi.
Bulaya amesema kutoa mafunzo ya silaha kwa Vijana wengi wakati hawapati nafasi za kujiunga na Jeshi hilo inaweza kupelekea baadhi yao kutumia mafunzo waliyopata kufanya uhalifu.
Aidha, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias Kwandikwa, amesema Jeshi hutoa mafunzo ya silaha kwa Vijana katika idadi inayotakiwa na mafunzo ya JKT yanalenga kuwajengea Vijana uwezo wa kujitegemea badala ya kuajiriwa.