Bunge la ‘Congress’ la nchini Marekani limemzawadia rais mpya wa nchi hiyo, Joe Biden cheti maalum cha ushindi baada ya kupata kura 306 na kuthibitishwa kuwa rais wa 46 wa Marekani kuanzia Januari 20 mwaka huu.
Hafla hiyo imefanyika ikiwa ni saa moja tangu wafuasi wa Donald Trump walipovamia bunge hilo kisha kufanya vurugu zilizopelekea vifo vya watu wanne na kujeruhi zaidi ya 50.
Hatua hii inaashiria kukamilika rasmi kwa uchaguzi wa Marekani na kuwahakikishia Biden na Harris kuapishwa hapo Januari 20, licha ya jitihada za Trump kuzuia kufanikiwa kwa tukio hilo.
Rais anayemaliza muda wake, Donald Trump ametoa kauli kuwa anakubaliana na uamuzi wa bunge licha ya kutokubaliana na matokeo ya uchaguzi huo, akiahidi kuwa kutakuwa na makabidhiano ya madaraka kwa njia ya amani hapo Januari 20.