Bunge la Ghana limepitisha mswada wenye utata wa kupambana na LGBTQ+ baada ya takriban miaka mitatu ya majadiliano.
Mswada huo mpya unaweka kifungo cha hadi miaka mitatu jela kwa yeyote atakayepatikana na hatia ya kujitambulisha kama LGBTQ+.
Pia inaweka kifungo cha juu zaidi cha miaka mitano jela kwa kuunda au kufadhili vikundi vya LGBTQ+.
Mswada huo uliidhinishwa kwa kauli moja Jumatano kufuatia kukamilika kwa usomaji wa tatu. Mapendekezo ya marekebisho ya muswada huo yalikataliwa na Spika, Alban Bagbin, wakati wa kikao hicho.
Wabunge walipuuza majaribio ya kubadilisha vifungo vya jela na huduma za jamii na ushauri.
Ni ishara ya hivi punde ya kuongezeka kwa upinzani dhidi ya haki za LGBTQ+ katika taifa hilo la kihafidhina la Afrika Magharibi.
Mswada huo sasa unatarajiwa kupelekwa kwa Rais Akufo-Addo ili apate kibali chake cha kutiwa saini na kuwa sheria.