Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embalo ameamua kulivunja Bunge linalotawaliwa na upinzani siku ya Jumatatu, siku tatu baada ya matukio aliyoyataja kama “jaribio la mapinduzi”, limebaini agizo la rais lililotumwa kwa vyombo vya habari.
Tarehe ya uchaguzi ujao wa wabunge itatangazwa kwa wakati ufaao, kwa mujibu wa sheria ya Katiba,” agizo la rais limeongeza. Rais Embalo ametaja “njama” kati ya kikosi cha walinzi wa taifa na “baadhi ya wanasiasa katika serikali”.
“Baada ya jaribio hili la mapinduzi lililoongozwa na kikosi cha walinzi wa taifa na mbele ya ushahidi mkubwa wa kuwepo kwa ushirikiano wa kisiasa, utendaji wa kawaida wa taasisi za Jamhuri hauwezekani. Mambo haya yanathibitisha kuwepo kwa mgogoro mkubwa wa kisiasa ,” agizo la rais limesema.