Bunge la Liberia lilipiga kura Jumatano kuidhinisha kuundwa kwa mahakama ya uhalifu wa kivita, miaka ishirini baada ya mzozo wa umwagaji damu mkubwa zaidi katika historia ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
Liberia ilikumbwa na vita viwili vya wenyewe kwa wenyewe kati ya 1989 na 2023 ambapo ukatili mkubwa ikiwa ni pamoja na mauaji, ubakaji, na matumizi ya askari watoto yalifanyika.
Kamati ya ukweli na maridhiano ilipendekeza kuanzishwa kwa mahakama maalum ya kuwahukumu watuhumiwa wa uhalifu lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.
Pendekezo la kuunda mahakama hiyo liliibuliwa na Rais mpya Joseph Boakai na kuungwa mkono na wabunge 42 kati ya 72. Ili kutekelezwa, ni lazima azimio hilo liidhinishwe na seneti.
Hakuna tarehe iliyowekwa ya kura ya seneti.
Vita hivyo viwili vya wenyewe kwa wenyewe viliua takriban watu 250,000.
Viongozi wa awali wa Liberia wamejiepusha na kuanzisha mahakama kwa kile wanaharakati wanasema ni kutaka kujikinga wenyewe au wafuasi wao dhidi ya mashtaka.