Bunge la Seneti nchini Kenya limeanza mchakato wa kusikiliza na kujadili mswada wa kutimuliwa ofisini kwa naibu wa Rais katika taifa hilo la Afrika Mashariki Rigathi Gachagua.
Mchakato huu unaendelea muda mfupi baada ya mahakama kwa mara nyengine kutupilia mbali ombi la Gachagua la kutaka bunge la Seneti kuzuiliwa kuujadili mswada wenyewe.
Katika tukio la kihistoria wiki iliopita, bunge la kitaifa lilipiga kura kuidhinisha mchakato wa kutimuliwa kwa Rigathi kwa makosa 11 ikiwemo ufisadi na kutumia vibaya madaraka
Rigathi mwenye umri wa miaka 59 amekanusha madai yote anayokabiliwa nayo na ataendelea kuhudumu katika wadhifa wake hadi pale ambapo bunge la Seneti litaamua kuhusiana na kesi yake