Wabunge 363 waliokuwepo bungeni mjini Dodoma leo Jumanne Machi 30, 2021 wamepiga kura za ndio kumthibitisha Dk Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania.
Dkt. Mpango amethibitishwa baada ya kupendekezwa na Rais Samia Suluhu Hassan na jina lake kusomwa bungeni mjini Dodoma na Spika Job Ndugai.
“Naomba kutangazia Bunge hili na nchi yetu kwa ujumla kwamba kura za hapana hakuna hata moja, kura zote 363 ni kura za ndiyo kwa hiyo amepata asilimia 100 ya kura zote.” Ndugai
“Kufuatana na ibara ya 49 makamu wa rais kabla ya kushika madaraka yake ataapishwa mbele ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji kazi wake kwa tarehe itakayopangwa makamu wa rais mteule ataapishwa,” Ndugai.